Serikali ya Tanzania na Taasisi ya African Institute for Mathematical Sciences - Next Einstein Initiative (AIMS-NEI) wamesaini Mkataba wa Makubaliano kuanzishwa kwa kampasi ya taasisi hiyo nchini itakayofundisha na kuendeleza masomo ya Hisabati na Sayansi.
Mkataba huo umesainiwa   jana na Katibu Mkuu wa   Wizara ya Elimu na Mafunzo  ya Ufundi, Profesa Sifuni Mchome kwa upande
wa Serikali na  Bwana Thierry Zomahoun,
Mkurugenzi Mtendaji wa AIMS-NEI 
jijini  Dar es Salaam.
Profesa Mchome amesema kusainiwa
kwa mkataba huo ni  jitihada za Mheshimiwa
Rais Jakaya Kikwete kuhakikisha kuwa Taifa linakuwa na wataalam wa kutosha
katika Nyanja za Hisabati na Sayansi. Mheshimiwa Rais alikutana na kufanya
mazungumzo na viongozi wa taasisi hiyo alipokuwa ziarani nchini Canada mwishoni
mwa mwaka jana.
Akizungumzia mkataba huo,
Profesa Mchome alisema “Hii ni nafasi ya pekee maana huwezi kupata Mainjinia
bila kujua hesabu, wala Madaktari na Wanasheria bila kuwa na ufahamu wa hesabu,
na hesabu ndiyo kila kitu,”.
Taasisi ya African Institute for Mathematical Science-Next
Einstein Initiative (AIMS-NEI), wameshafungua kampasi zake  katika  nchi za Afrika Kusini, Senegal, Ghana na
Cameroon, na kwa hapa Tanzania tayari wamepata eneo wilayani Bagamoyo katika
majengo ya Boma ambayo yatakarabatiwa. Kwa kuanzia masomo hayo yatatolewa
katika Chuo Kikuu cha Nelson Mandela kilichopo Arusha ambapo wanafunzi 40 wa
awali wameshadahiliwa tayari kwa kuanza masomo hayo mwezi Septemba mwaka huu.
Mkurugenzi Mtendaji wa African Institute for Mathematical Sciences-Next
Einstein Initiative (AIMS-NEI), Thierry Zomahoun, alisema Tanzania ni
miongoni mwa nchi bora kiuchumi katika ukanda wa Afrika Mashariki, ili ijijenge
katika misingi ya uchumi imara zaidi, haina budi kuwekeza katika masuala ya
hesabu na sayansi ili kupata watalaamu 
watakaolisaidia taifa kusonga mbele kimaendeleo.
 
 EVENT ;
EVENT ;