Tuesday 5 August 2014

Viongozi wa Afrika wakutana Marekani

Takriban viongozi hamsini kutoka nchi za Afrika wanatarajiwa kuhudhuria mkutano wa siku tatu utakaohitimshwa Jumatano.
Mkutano huo wa Marekani na viongozi 50 wa nchi za Afrika uliandaliwa na idara ya biashara ya Marekani.http://www.bbc.co.uk/swahili/habari/2014/08/140805_afrika_marekani_viongozi.shtml

Katibu wa maswala ya Biashara wa Marekani Penny Pritzker amesema kuwa tangazo rasmi litatolewa kwenye mkutano huo kuhusiana na takriban dola milioni 900 zitakazotolewa kwa mipango ya kibiashara.
Hayo yakijiri, Marais watatu, rais wa Liberia, wa Guinea, na wa Sierra Leone wamevunja safari zao kuhudhuria mkutano huo kufuatia janga la Ebola.
Ebola imesababisha vifo vya watu Zaidi ya 800 katika kanda ya Afrika Magharibi kwa ujumla.
Kufanyakia kwa mkutano huu ni kutimia kwa ahadi ya Rais Obama aliyotoa mwaka uliopita alipozuru nchi tatu za Afrika Senegal, Tanzania, na Afrika Kusini.
Kongamano hilo litaangazia biashara kati ya Marekani na Bara la Afrika. Kwa mujibu wa mhariri wetu China inaongoza kwa kiwango cha biashara wanayofanya na nchi za Afrika

Mlipuko wa homa ya Ebola umelazimisha rais kukatiza safari yake Marekani
China inafanya biashara ya takriban dola bilioni 200 na bara la Afrika. Kiwango hicho ni Zaidi ya maradufu kiwango cha biashara ya Marekani na nchi za bara Afrika.
Ingawa China imeongoza, kulingana na utafiti wa Shrika la Fedha Duniani, China ina uhusiano wa kibiashara nan chi chache tu.
China inafuatiwa na Japan, India na Ulaya.
Hayo yakijiri, Ghana imesema itatafuta msaada kutoka kwa Shirika la fedha duniani (IMF) ili kuimarisha uchumi wao kwani Ghana imekuwa kati ya nchi zilizovuta mkia kiuchumi kote ulimwenguni mwaka huu.
Mwaka 2013, 67% ya biashara ya Afrika na Marekani ilifannywa na nchi tano tu - Nigeria, South Africa, Angola, Misri and Algeria.
Marekani hununua bidhaa nyingi kutoka nchi hizi inapolinganishwa na bidhaa wanazouzia nchi hizo. Mafuta huchangia Zaidi ya asilimia hamsini ya bidhaa zinazouzwa kwenda Marekani.
Takrimu za uwekezaji wa kigeni wa moja kwa moja (FDI) figures zinaonyesha mtindo fulani – mwaka 2012 74% ya fedha zilizowekezwa na nchi za kigeni barani Afrika ziliendea nchi tano - Nigeria, Afrika kusini, Misri, na Algeria huku Mauritius ikichukua nafasi ya Angola na kuwa nchi ya tano katika orodha hiyo.
Mwaka 2011, 75% ya bidhaa zilizouzwa kwenda China kutoka nchi zilizo kusini mwa Jangwa la Sahara zilitoka nchi tano tu, huku nchi sita zikichukua Zaidi ya 80% ya bidhaa zilizouzwa na China barani Afrika.

Ghana inalenga kupata msaada kufadhili miradi yake ya kawi
Huku zaidi ya nchi hamsini zikitarajia kufaidika kutoka kwa mkutano wao na rais wa Marekani Barck Obama, kuna nchi ambazo hazikualikwa - Jamhuri ya Afrika ya Kati, Eritrea, Sudan na Zimbabwe.
Waziri wa habari wa Zimbabwe Jonathan Moyo alipuuzilia kutoalikwa na Marekani kuhudhuria mkutano huo wa Viongozi wa Afrika kuwa “si jambo.”
“Tunaelewa kuwa Marekani inalenga kutimiza matakwa yake, na inahofia kuwa Uchina imekuwa kwa haraka na kuongoza katika mahusiano na Afrika,” Mugabe aliarifu Gazeti linalomilikiwa na taifa, Herald.
Watakaohudhuria wameandaliwa chajio na Rais Obama, White House, baada ya mkutano wa leo.
Mada zitakazoangaziwa kesho (Jumatano) ni biashara, usalama, na uongozi.
Wanaokosoa kongamano hilo wamesema kuwa Obama hakufanya mikutano ya moja kwa moja na marasi wan chi za Afrika.

Bwana Kerry alikutana na waziri mkuu wa Libya Libyan Abdullah al-Thinni
Kualikwa kwa Rais Yoweri Museveni kumevutia wanaharakati wa haki za wanaofanya mapenzi ya jinsia moja baada ya Museveni kuidhinisha, mapema mwaka huu, muswada ulioweka adhabu kali dhidi ya wanaofanya mapenzi ya jinsia moja.
Mara kwa mara, Obama,ameshutumiwa kwa kupuuza uhusiano wa Marekani na bara la Afrika huku ikizingatiwa kuwa Obama ni Rais wa kwanza ambaye ni Chotara wa Mwafrika na Mmarekani.
Kando na ziara ya Obama mwaka uliopita, Obama amezuru mara mbili nchi zilizo kusini mwa jangwa la Sahara, katika kipindi chake cha uongozi. Alipitia Ghana kwa muda mfupi, Julai 2009, na pia kuhudhuria mazishi ya hayati Nelson Mandela, shujaa wa Afrika kusini.