Wednesday, 6 August 2014

ELIMIKA TANZANIA YA FUNGUA OFISI YAKE MPYA

ETA leo imefungua ofisi mpya mtaa wa Lumumba wilaya ya Ilala jijini dar es salaam.ofisi imefunguliwa na Mwenyekiti wa ETA Mh.Mwemezi Kaijage huku  akiwaasa viongozi na wanachama kushilikiana na kutokata tamaa pale changamoto zinapo wakabili.

 

 Mlezi wa ETA pia amewashauli vijana kuwa makini na kuwa waaminifu katika maisha yao ,pia kudunisha upendo na aman miongoni mwao,amesema hayo huku akitoa mifano hai juu ya maisha yake na changamoto alizopitia.

Wakielezea kwa furaha juu ya tukio hilo wanachama na viongozi walitoa shukulani zao za zati kwa mlezi huyo ,pia kumshukulu Mwenyekiti kwa kutimiza lengo la kuwa na ofisi yao.
Wakipongezana ofisin hapo wanachama wame toa haadi mbalimbali ikiwemo kudumisha ushirikiano na mshikamano miongoni mwao ,pia kuendeleza kwa umakini miradi yote ya  ETA.
   
ETA inakaribisha vijana wengine kujiunga nao ili kuendeleza kutoa Elimu ya urahia,uchumi na kujitegemea kwa jamii .Pia ETA inatalajia kutoa semina ya ujasiliamali ,uchumi ,urahia na kujitegemea kwa vijana hapa dar es salaam.