Wizara  ya 
Elimu na Mafunzo  ya  Ufundi 
kwa kushirikiana  na Asasi  za vyuo na 
taasisi za Canada wameanzisha Mpango wa kutekeleza mradi  wa 
Mafunzo  ya kukuza  stadi kwa ajili ya uajiri (improving skills
training for employment programme - ISTEP ). Mpango huu utajenga uwezo wa asasi
za Mafunzo ya ufundi nchini kufundisha kwa umahiri stadi zinazoitajika katika
sekta za uchimbaji wa madini, mafuta, gesi na sekta ya utalii.
Kaimu  Mkurugenzi wa Idara ya Ufundi na Mafunzo ya ufundi
stadi katika Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Thomasi   Katebalirwe 
alieleza hayo jijini Dar es Salaam katika warsha   ya makubaliano  na wadau 
iliyokuwa  ikijijadili hatua  mbalimbali 
katika kujenga  ushirikiano wa
jinsi wanafunzi  na tasnia
zitakavyofaidika na mpango huu.
Alisema  Mradi 
huu  utajikita  katika sekta  
za madini, gesi  na utalii,
kwamba  utajenga uwezo wa asasi za kitanzania
za Mafunzo ya ufundi kufundisha kwa umahiri stadi zinazohitajika katika sekta
zote za uchimbaji wa madini, mafuta na gesi na sekta ya utalii, na hivyo
kuwapatia vijana takribian 1,200 stadi mwafaka zitakazowawezesha  kujiajiriwa kwenye sekta ya uchimbaji na
utalii ama kujiajiri.
“Tayari
wataalanu wamefanya   upembuzi   katka 
maeneo  mbalimbali  , ili 
kupata    mahitaji  ya utekelezaji  wa mradi huo wa miaka  mitano, ambao utagharamia Dola za Canada million  13   na
utawanufainisha  watanzania   12,000 hasa 
katika  masuala  ya gesi .” alisema Katabalirwe.
Aidha,    alisema 
taasisi  11  zitashirikiana katika kukuza uelewa  kwa vijana  
kwa kuwa  gesi  ni kitu kipya 
kinachohitaji nguvu  kazi  ya kutosha na yenye Mafunzo maalum. Vijana
hao watatoka katika taasisi za utalii, Madini na Gesi ambao watapatiwa Mafunzo
ya uchimbaji wa madini na uchomeleaji wa mabomba ya gesi.  
Mwenyekiti  kutoka shirikisho  la wachimbaji na watafutaji  wa Madini Tanzania , Nyanda  Shuli 
alisema  mpango huo  ni muhimu 
katika  kuendeleza  Sekta 
ya  Madini    na Nishati 
kwa kuwa inahitaji   nguvu
kazi  ya kutosha  kukuza 
sekta  hiyo.
 
 EVENT ;
EVENT ;