Mama wa kupangisha bi Chanbhua akiwa na mwanawe (Gammy)
![](https://lh3.googleusercontent.com/blogger_img_proxy/AEn0k_sAaSke0yTDTd8Dt4FEt_fz0H3F1HvEl0N7hiUIrUF-rZIV2lP82azh8xQj4-SrPWNkkz_x_2UomxZwwdo8kpQoBu2iPh0Kng8U_wpqLrplSLFP5n_x04J-DuGDcCCbxnK3sSU9YqHvYXvDKbRHLSzf2qZiTI8Q0yFkfhV523wc4mpHuOd5EV7VmYtH3faF6MUwTA2nCxUV4xl6F51gzo-SE_hPjX3YqH2M8udPUd5oSABp2B76fMwCykDByVijbpxCfAU8-QHgasHluLgjQB4Yt-KQ8zyjNCrzXHTUo76SihlU9u6_1NK6tg=s0-d) |
Familia moja kutoka Australia imekanusha kumtelekeza mtoto waliomlipa
mama mmoja nchini Thailand kuwabebea kufuatia ripoti za daktari kuwa
alikuwa na upungufu wa kiakili Pattharamon Chanbua, 21, aliingia mkataba wa kuwasaidia Waaustralia
hao kupata mtoto baada ya mwanamke huyo kushindwa kubeba mimba
mwenyewe.
Hata hivyo alipojaaliwa akazaa
mapacha wazazi hao walikuja wakamchukua mmoja ambaye akili zake zilikuwa
timamu na wakamuacha nyuma mtoto Gammy baada ya ripoti ya daktari
kuonesha kuwa alikuwa na akili taahira.
Chanmbua anasema kuwa punde baada ya madaktari
kugundua kulikuwepo na hitilafu wazazi hao wa Gammy walimshauri aavye
mimba hiyo lakini akkataa kwani haiambatani na dini yake ya Kibudhaa.
Wazazi hao wa Gammy wamejitetea wakisema kuwa
walimchukua mtoto mmoja baada ya madaktari kutarajia kuwa Gammy angekuwa
na matatizo ya ugonjwa wa moyo na maambukizi ya mapafu.
Baba ya mapacha hao wawili aliwatembelea wote
wakiwa hospitalini punde baada ya kuzaliwa lakini haijulikani kwanini
alimtelekeza Gammy.
Mama huyo ambaye tayari yuko na wanawe wawili sasa anasema hatamtupa Gammy bali atamlea kama mwanawe.
Matukio hayo yamepelekea watu kote nchini Australia wanakotoka wazazi wake kufoka wakiwalaumu kwa kumnyima haki zake Gammy .
Aidha wengi wanakashifu matukio hayo wakidai
kuwa huo ni ukoloni mamboleo kwa watu wenye hela lakini wanamatatizo ya
kuwapata watoto wao wenyewe wanasafiri kuelekea nchi za mbali na
kukodisha wanawake maskini kwa niya ya kujitoa mzigo wa ukosefu wa
watoto.
![](https://lh3.googleusercontent.com/blogger_img_proxy/AEn0k_v6KniFDVOBAuQo1d5KoXXLqtFimOaXfwGHmqGm_l23tygxJXDnLharmsD9NwW_lCeKgJf2KIzyhTxF6BIUlGhzUio_knxn9Ge1IJWfUF0O9Bvn57XHUdhYjm6OSn_bQndi04jT8ZBft6GLFG7QX5mTxruEpZvZzFIu7Q6agvzmYTkluCBQvT61maAE5el4Iput0Ft0unlLnCM=s0-d)
Mtoto aliyezaliwa na akili taahira kwa mama wa kupanga .
Lakini wakipata watoto hao wanakasoro fulani wanatoroka na kuwaachia wale wazazi maskini na mzigo wa kuwalelea watoto wao.
Waziri mkuu wa Australia Tony Abbott na waziri
wa maswala ya uhamiaji nchini humo Scott Morris wamehuzunishwa na
tukio hilo wakisema ni la kushtua sana.
Wazazi wa Gammy wamenukuliwa katika mjadala na
runing moja ya Channel 9 wakisema kuwa wanamtoto mwenye umri wa miezi 6
lakini hawana mtoto mwengine na kukanusha habari kuwa walimtelekeza
ndugu ya mtoto wao wa kike.
Wazazi hao wanaoishi mjini Perth, vilevile wameiambia runinga ya taifa kuwa hawajui analosema bi Chanbhua .
Chanbua aliiambia jarida la Fairfax Media
kuwa babake Gammy anaumri wa miaka Hamsini hivi na kuwa aliwahi kuja
hospitalini na alionekana kumjali sana msichana wake na kumpuuza kabisa
Gammy licha ya kuwa alikuwa hapo kitandani.
''Alikataa hata kumtizama usoni mwanaye''
![](https://lh3.googleusercontent.com/blogger_img_proxy/AEn0k_tbuNI5i8KZs0NY2UJbzXF8rG08BKp9T0CQkvTqFca31ipKITkrBQbJZNa-u96P6oZR2rXLWBegwmWGytjWktKeExPV87dIccCVYOJD8gbiOP_rzkR1NAJ9PE6TaMgvIvebngG7AE0RfLWAHpcMF6bVWNQKuigFFlXijkwcK_Du9WdY8N_YZJElyM8Q1TYGjJpMrlD2olGy=s0-d)
Mtoto aliyezaliwa na akili taahira kwa mama wa kupanga .
''sasa nitafanya nini ilinipate kumlea ?
Labda itanibidi niwashtaki mahakamani ilinipate hela za kuwatunzia mtoto wao ''.
Waziri wa uhamiaji hata hivyo amesema kuwa
serikali ya Australia ikishirikiana na ile ya Thailand zinashirikiana
kutafuta suluhu ya mkasa huo .
Bwana Morris alisema kuwa mtoto Gammy ni raiya
wa Australia na kuwa anastahili kupata msaada wa kimatibabu kutoka kwa
serikali ya Australia.
Ni haramu kumlipa mtu iliakubebee mimba nchini
Australia kwa hivyo wazazi ambao hawana uwezo wa kupata mtoto hukimbilia
mataifa ya nje na kufanikisha azimio la kuwa wazazi.
Tayari wasamaria wema wamechangisha dola laki mbili kumsaidia mama huyo kumlea mtoto Gammy. | | | | |