Mkono wa Rubani uling'oka akitaka kutua kwa dharura.
Rubani mmoja nchini Uingereza
alipoteza mwelekeo angani akiendesha ndege ya biria baada ya mkono wake
wa bandia kuchomoka wakati alipokua akielekea kutua.
Rubani huyo wa shirika la ndege la Flybe mwenye umri wa miaka 46 , aliruka kutoka uwanja wa ndege wa Birmingham, akiwa na abiria wapatao 47 ndani yake, wakati alipokaribia kutua katika uwanja wa ndege wa mji wa Belfast alikumbana na upepo mkali angani ambao ulimsababisha atue kwa ghafla ilivyo bahati hakukuwa na madhara kwa ndege yenyewe wala abiria.
Ndege hiyo ilitua kwa mlio mkubwa ingawa hakuna mtu aliyejeruhiwa na pia ndege haikuharibika.
Rubani alisema atakuwa makini zaidi katika siku za usoni kuhusiana na mkono wake huo bandia.