Mama wa kupangisha  bi Chanbhua akiwa na mwanawe (Gammy) 
|  | 
| Familia moja kutoka  Australia imekanusha kumtelekeza mtoto waliomlipa 
mama mmoja nchini Thailand kuwabebea kufuatia ripoti za daktari kuwa 
alikuwa na upungufu wa kiakili Pattharamon Chanbua, 21, aliingia mkataba wa  kuwasaidia Waaustralia
  hao kupata mtoto baada ya mwanamke huyo kushindwa kubeba mimba 
mwenyewe. Hata hivyo alipojaaliwa akazaa 
mapacha wazazi hao walikuja wakamchukua mmoja ambaye akili zake zilikuwa
 timamu na wakamuacha nyuma  mtoto Gammy baada ya ripoti ya daktari 
kuonesha kuwa alikuwa na akili taahira.
 Chanmbua anasema kuwa punde baada ya madaktari 
kugundua kulikuwepo na hitilafu wazazi hao wa Gammy walimshauri aavye 
mimba hiyo lakini akkataa kwani haiambatani na dini yake ya Kibudhaa.
 Wazazi hao wa Gammy wamejitetea wakisema kuwa 
walimchukua mtoto mmoja baada ya madaktari kutarajia kuwa Gammy angekuwa
 na matatizo ya ugonjwa wa moyo na maambukizi ya mapafu.
 Baba ya mapacha hao wawili aliwatembelea wote 
wakiwa hospitalini punde baada ya kuzaliwa lakini haijulikani kwanini 
alimtelekeza Gammy.
 Mama huyo ambaye tayari yuko na wanawe wawili  sasa anasema hatamtupa   Gammy  bali atamlea kama mwanawe.
 Matukio hayo yamepelekea  watu kote nchini Australia wanakotoka wazazi wake kufoka  wakiwalaumu  kwa kumnyima haki zake Gammy .
 Aidha wengi wanakashifu matukio hayo wakidai 
kuwa huo ni ukoloni mamboleo kwa watu wenye hela lakini wanamatatizo ya 
kuwapata watoto wao wenyewe wanasafiri kuelekea nchi za mbali na 
kukodisha wanawake maskini kwa niya ya kujitoa mzigo wa ukosefu wa 
watoto.
 
 
                        Lakini wakipata watoto hao wanakasoro fulani wanatoroka na kuwaachia wale wazazi maskini na mzigo wa kuwalelea watoto wao.
 
Mtoto aliyezaliwa na akili taahira kwa mama wa kupanga .   Waziri mkuu wa Australia  Tony Abbott na waziri 
wa maswala ya uhamiaji nchini humo  Scott Morris wamehuzunishwa  na 
tukio hilo wakisema ni la kushtua sana.
 Wazazi wa Gammy wamenukuliwa katika mjadala na 
runing moja ya Channel 9 wakisema kuwa wanamtoto mwenye umri wa miezi 6 
lakini hawana mtoto mwengine na kukanusha habari kuwa walimtelekeza 
ndugu ya mtoto wao wa kike.
 Wazazi hao wanaoishi  mjini Perth, vilevile wameiambia runinga ya taifa  kuwa hawajui analosema  bi Chanbhua .
 Chanbua  aliiambia jarida la Fairfax Media 
kuwa babake Gammy anaumri wa miaka Hamsini hivi  na kuwa aliwahi kuja 
hospitalini na alionekana kumjali sana msichana wake na kumpuuza kabisa 
Gammy licha ya kuwa alikuwa hapo kitandani.
 ''Alikataa hata kumtizama usoni mwanaye''
 
 
                        ''sasa nitafanya nini ilinipate kumlea ?
 
Mtoto aliyezaliwa na akili taahira kwa mama wa kupanga .   Labda itanibidi niwashtaki mahakamani ilinipate hela za kuwatunzia mtoto wao ''.
 Waziri wa uhamiaji hata hivyo amesema kuwa 
serikali ya Australia ikishirikiana na  ile ya Thailand zinashirikiana 
kutafuta suluhu ya mkasa huo .
 Bwana Morris alisema kuwa mtoto Gammy ni raiya 
wa Australia na kuwa anastahili kupata msaada wa kimatibabu kutoka kwa 
serikali ya Australia.
 Ni haramu kumlipa mtu iliakubebee mimba nchini 
Australia kwa hivyo wazazi ambao hawana uwezo wa kupata mtoto hukimbilia
 mataifa ya nje na kufanikisha azimio la kuwa wazazi.
 Tayari wasamaria wema wamechangisha dola laki mbili kumsaidia mama huyo kumlea mtoto Gammy.
 |  |  |  |  |